MHE. MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI AHITIMISHA KAMPENI KATA YA MATWIGA CHUNYA

 


Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya ameendelea na kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ikiwa ni siku ya mwisho ya kampeni.

Leo hii amefanya kampeni Vijiji vya Isangawana,Mazimbo na Matwiga Kata ya Matwiga huku akiwasisitiza wananchi kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwani ndiyo watakaowaletea maendeleo.

Amesema miradi mingi inatekelezwa nchini hivyo wananchi wawahi mapema Vituo vya kupigia kura ili wapige kura kuwachagua viongozi wa vitongoji na Vijiji.



Post a Comment

0 Comments