Waziri wa Madini *Mhe Anthony Mavunde* akiongozona na Mkuu Wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya , Mbunge wa Lupa *Mhe. Masache Kasaka* na viongozi wa CCM na Serikali, wamefika na kukagua Mto zira uliopo Kata ya Ifumbo.
Ukaguzi wa mto huo umefanyika ili kuona Athari za Kimazingira zinazotokana na uchimbaji wa Dhahabu ndani ya Mto huo. Waziri Mavunde ametoa agizo la kusitishwa shughuli zote ndani ya Mto huo na kuunda Tume Jumuishi itakayokagua na kuleta Taarifa kwake kwa Maamuzi zaidi.
UJENZI WA CHUNYA NI JUKUMU LETU SOTE


0 Comments