MWEF YATOA MSAADA HOSPITALI YA WAZAZI META

  


NA MWANDISHI WETU, MBEYA

Taasisi ya Maryprisca Women Impowerment Foundation(MWEF)inayoongozwa na Naibu Waziri wa  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa ajili ya kutoa msaada kwa wazazi waliojifungua siku ya sikukuu ya Christmas.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Maryprisca Women Impowerment Foundation Adam Simbaya amesema lengo la kutembea Hospitali ya wazazi Meta ni kumshukuru Mungu pia akianisha zawadi zilizotolewa kuwa ni pamoja na maziwa, sabuni,pampas na wipes.

Aidha Simbaya amesema wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye amekuwa akiyagusa makundi mbalimbali yakiwemo ya wanawake na watoto.

Scolastica Kapinga ni muuguzi wa zamu kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Kitengo cha Wazazi Meta ameishukuru Taasisi hiyo kwa kutoa msaada kwa wazazi na watoto sanjari na maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali yamefanya watoe huduma kwa ufanisi mkubwa.

Post a Comment

0 Comments