MHE. MWANTONA NI TUMAINI TIMILIFU JIMBO LA RUNGWE

Tuendako Majimboni.

Na Gordon Kalulunga

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu tarajali mwaka huu 2025 ambao utahusisha wataka Urais, Ubunge na Udiwani, nimeanza kutembea katika Majimbo kusikiliza na kuona Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kwa viongozi wanaoenda kuhitimisha/kuanza upya katika nafasi zao.

Wataalam wa ligi za Siasa wanasema uzoefu unaonesha kwamba, ni rahisi sana kumg'oa Diwani au Mbunge aliyehudumu kwa miaka 10 katika nafasi hiyo kuliko Diwani au Mbunge aliyehudumu kwa miaka Mitano.

Leo tuangazie Kata ya Kiwira iliyopo katika Jimbo la Rungwe Mkoani Mbeya na Mbunge wa Jimbo hili ni Mhe. Antony Albert Mwantona.

Sifa Moja wapo ya Mbunge huyu baadhi ya wananchi wanasema ni kiongozi mwenye shukrani na anayemiliki masikio zaidi kuliko mdomo yaani anatajwa kuwa ni msikivu kwa wananchi bila kujali hali zao Wala itikadi zao za Siasa.

Katika Kata hii ipo miradi kadhaa iliyotekelezwa ikiwemo nyanja za Afya, Elimu, Maji na uchumi.

Wananchi wa Kiwira wanasema Mbunge huyo baada ya kuingia madarakani na kuwasikiliza wananchi mahitaji yao alianza kutekeleza kwa uhakika ahadi zake kwa kushirikiana na wananchi wenzake.

Wanasema aliwapelekea Mabati 204 kwa ajili ya kuezeka Zahanati Yao iliyopo eneo la Kanyegele.

Katika Kijiji cha Kikota aliwapelekea Bati zaidi ya 100 kwa ajili ya ujenzi huku akipeleka mifuko ya Saruji 100 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Ukukwe.

Wanayataja mambo wanayoyakumbuka kwa kusema Mbunge huyo ameshiriki nao pia katika kutatua kero ya Maji ktoa Milioni 40 ujenzi wa Tank la Maji lililopo eneo la New Land huku mradi wa Maji Mpandapanda ukiwa unasonga kwa Milioni 500.

Pia wanayataja Makaravati Manne kuwa yalitolewa na Mbunge huyo kwa ajili ya eneo la Kikota na zaidi wanasema hawawezi kusahau mradi wa Maji Kanyegele na uanzishwaji wa ujenzi wa Soko la Mazao eneo la Karasha.

Kwa uchache leo tutamatike kupitia miradi hii ambayo imeisisimua Kata ya Kiwira na ndiyo maana ninasema kuwa, Tuendako Majimboni Mhe. Antony Mwantona ni Tumaini Timilifu katika Jimbo la Rungwe 2025.


0765615858

Post a Comment

0 Comments