SOPHIA MWAKAGENDA MBUNGE ALIYESHIKAMANA NA WANANCHI

 

Na Tata Gordon Kalulunga 

MHESHIMIWA Sophia Hebron Mwakagenda ni Mbunge wa Viti maalum Mkoani Mbeya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Pia aliwahi kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Rungwe Mkoani Mbeya.

Pamoja na kura kutokutosha, wananchi wanasema ameendelea kutenda kazi zake za Ki-bunge kwa wanawake wa Mkoa huo.

Kwa Jimbo la Rungwe Sophia Mwakagenda ameendelea kutajwa vema kutokana na kazi zake na utu wake kwa wananchi.

Baadhi wanasema anayoyafanya Mbunge huyo kwa wananchi huenda angekuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) angakuwa anafanya zaidi.

Duru za Siasa zinamtaja Mhe. Sophia kuwa huenda atawania tena Ubunge wa Jimbo la Rungwe lakini kikwazo kinaweza kuwa ndani ya chama chake ambako mpaka sasa Wabunge 19 walioko Bungeni kupitia Chadema ni kama hawajui hatima yao.

Lakini yeye Mhe. Sophia ameendelea kushikamana na wananchi.

Post a Comment

0 Comments