Jumla ya Wilaya 139 nchini kufikiwa na huduma ya mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na mpaka sasa Wilaya 108 tayari zimefikiwa huku Wilaya 31 zilizosalia nazo zikitarajiwa kupata huduma ya mkongo wa Taifa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akihitimisha ziara ya kikazi Mkoani Pwani ziara iliyoanzia Mkoa wa Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amempongeza na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Hassan kwa namna anavyoiwezesha Kampuni ya simu nchini (TTCL)kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kidijitali sanjari na kutoa huduma hiyo nchi ya Congo ,Afrika nzima hata ulaya kwa kupitia baharini.
Aidha maboresho makubwa yanaendelea kufanywa na Serikali kwa ushirikiano na mashirika ya ndani na nje ya nchi kutaifanya Tanzania kutokuwa kisiwa.
Endapo mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utakamilika utapanua wigo kibiahara ndani na nje ya nchi.






0 Comments