Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa katika kumjengea mwanamke uwezo wa kiuchumi na kijamii ikiwemo hatua ya Uwezeshaji wa kifedha kupitia mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) ambao umewawezesha wanawake kupata mikopo kwa masharti nafuu kupitia biashara zao.
Ameyasema hayo katika hafla ya Mwanamke Kwanza akiwa mgeni rasmi hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam huku akiwahimiza wanawake kupitia mijadala wanapata maarifa mapya na mbinu bora za kuimarisha biashara zao.
Aidha amesema mijadala inawapa fursa ya mitandao ya kibiashara na kujadili changamoto kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi huku akipongeza juhudi za wanawake kupiga hatua kiuchumi,kisiasa,teknolojia na sekta mbalimbali.
Hata hivyo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameupongeza uongozi wa Tudima Events chini ya uongozo wa Bi Enna Kiondo ambapo lengo la jukwaa la ni kuwakomboa wanawake kifikra na kiuchumi.





0 Comments