KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI IMETOA MAELEKEZO HAYA IKIWA CHUNYA MBEYA

 


Na Mary Mwaisenye, Chunya

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeshauri Shirika la Madini la Taifa  (STAMICO ) kuweka mazinga wezeshi kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu ili kuwezesha kufurahia huduma wanazozitoa katika kituo cha mfano kilichopo mtaa wa Itumbi kata ya Matundasi mamlaka ya mji mdogo Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.

Akitoa kauli hiyo marchi 14 2025 kwaniaba ya kamati,Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini David Mathayo amesema wahakikishe huduma wanazozitoa hazwauizi wachimbaji wadogo ili waweze kunufaika na kituo hicho.

Wakati huo huo Kamati imesisitiza STAMICO kuhakikisha wanatunza mazingira yanayozunguka kituo na kuendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo juu ya matumizi sahihi ya baruti.

Awali Meneja wa Shirika la Madini Taifa (STAMICO) Nchagwa Chacha akitoa taarifa kwa Kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati Madini amesema kwa kipindi cha Julai 2023 hadi January 2025 wachimbaji wadogo wapatao 24 wamweza kupatiwa huduma kituoni hapo ambapo Tani 1521 za mbale ya dhahabu zimeletwa kituoni kwaajili ya uchenjuaji katika mtambo wa CIP na kuhomwa kwa awamu 40.

Ambapo amesema kuwa jumla ya gramu 20,125.80 zimezalishwa zenye thamani ya sh.3.274 bilioni hivyo kweza kuwezesha serikali kupata mapato.


Mbali na wachimbaji wadogo kufika kituoni hapo kwaajili ya kujifunza na kufuata huduma za uchenjuaji pia wachimbaji wawili ambao ni Finta Processing Plant na Lisa Resources Limited wameweza kuiga teknolojia ya kituo na kwa kujenga mitambo ya CIP kama iliyo kituoni hapo.

Kamat ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imetembelea kituo cha cha mfano kwa wachimbaji wadogo kilichopo mtaa wa Itumbi kata ya Matundasi mamlaka ya mji mdogo Makongolos na soko kuu la madini wilaya ya Chunya ambapo wamesisitiza suala la usalama wakati wananafanya biashara zao sanjali na kuongeza kamera za usalama sokoni. 

Post a Comment

0 Comments