Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wanafunzi wa Vyuo nchini kusoma kwa bidii badala ya kuendekeza anasa wawapo masomoni.
Mahundi hayo katika madhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mbeya(CUoM).
Katika hatua nyingine Mahundi amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyowapambania wanawake nchini katika nyanja mbalimbali zikiwemo za uongozi hivyo amewahimiza wanawake na wanaume kumpa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Profesa Ernest Kitindi amesema ujumbe uliotolewa na mgeni rasmi umekuja kwa wakati na wanachuo wakizingatia watafika mbali zaidi.
Profesa Aulelia Temba amesema historia ya maadhimisho ya wanawake Duniani yaliasisiwa nchini Marekani na yameleta mabadiliko makubwa kwa wanawake Duniani,
Aidha Mkuu wa Chuo Profesa Romuald Haule amesema awali wanawake wamefanya matendo ya huruma katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya kwa kuvya usafi,pampas ba taulo za kike,
Neno la shukurani limetolewa na Mwenyekiti wa maandalizi Nomaliza Goliama ambaye amemshukuru mgeni rasmi kwa kuitikia wito wao.
Dhima kubwa katika maadhimisho hayo ni maadili na uchumi kwa wanawake ambapo wakufunzi mbalimbali wametoa mada





0 Comments