MBUNGE MASACHE AWAPA TABASAMU WANAWAKE CHUNYA

 


LUPA 📍

March 5,2025

NA MWANDISHI WETU

 Mbunge Jimbo la Lupa Mh Masache kasa ameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Mwanamke duniani ambapo kiwilaya yamefanyika ukumbi wa halmashauri saapanjo ambapo mgeni Rasmi ni Mh Merryprisca Mahundi Naibu Waziri wa Mawasiliano.


Kupitia maadhimisho hayo Mhe. Masache Kasaka ameelezea utekelezaji wa miradi mbalimbali afya, kilimo, elimu, maji, miundombinu na nishati pamoja na mikopo inayotolewa na halmashauri ya chunya.

Sambamba na hilo Mh.Masache Kasaka ametoa mitungi midogo ya gesi 100 kwa ajili ya Mama Lishe na kiasi cha *Tsh.3,000,000/=

Pia Mh Masache Kasaka ametumia muda huo kumshukuru Mh.Dkt Samia Suluhu Rais wa JMT kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali katika jimbo la Lupa-Chunya.

SAMIANAMASACHE

CHUNYAKAZIINAENDELEA

Post a Comment

0 Comments