MHE. MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI AFUTURISHA WANAFUNZI 135 WA KIISLAMU MBEYA SEKONDARI

  


NA MWANDISHI WETU, MBEYA

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amefuturisha wanafunzi 135 wa dini ya Kiislamu kwa lengo la kuwatia moyo katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameguswa na wanafunzi hao kufanya ibada ya funga kwani kupitia ibada ya funga watakuwa waadilifu pia uzingativu katika masomo yao.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametiwa moyo hivyo ameahidi kufuturisha vipindi vitatu vya funga ya Ramadhan.

Mkuu wa Shule Mwalimu Francis Mwakihabha amemshukuru Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa moyo wake wa ukarimu kwa wanafunzi.

Yahya Issah mwakilishi wa wanafunzi amemshukuru Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kuunga mkono ibada ya funga na kumuombea thawabu mbele za Mungu.

Aidha amemuomba kuwakumbuka pia wanafunzi wa Kikristo na wale wenye mahitaji maalumu ili nao washirikiane vema ibada ya funga.

Diwani wa Kata ya Mbalizi Road Mheshimiwa Adam Simbaya amesema moyo uliofanywa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari unapaswa kuigwa pia ameushukuru uongozi wa Mbeya Sekondari kwa kumpokea mgeni.



Wanafunzi hao 135 waliofuturushwa ni wa jinsi zote kutoka kidato cha kwanza hadi cha sita.

Post a Comment

0 Comments