MBUNGE MASACHE 𝗔𝗪𝗔𝗧𝗘𝗠𝗕𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗠𝗔𝗝𝗘𝗥𝗨𝗛𝗜 𝗪𝗔 𝗔𝗝𝗔𝗟𝗜 𝗠𝗕𝗘𝗬𝗔

 

Mbunge wa Lupa-Chunya Mhe. Masache Kasaka amewatembelea majeruhi wa ajali iliyohusisha basi la CRN na Gari la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya iliyosababisha vifo vya watu wanne na majeruhi watano.

Miongoni mwa majeruhi waliotembelewa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ni pamoja na Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya Lucia Sule, Waandishi wa Habari Epmacus Kalokola,Denis George na Seleman Ndelage.

Mheshimiwa Mbunge Masache ameipongeza Serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan ilivyowekeza vifaa tiba hivyo kuokoa gharama kubwa za Matibabu kwenda hospitali nje ya Mkoa wa Mbeya.

Post a Comment

0 Comments