Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amefika kutoa pole kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake Taifa(UWT) Mheshimiwa Mary Pius Chatanda aliyefiwa na Dada yake marehemu Losca Mwakyoma Mtaa wa Mwantegule Kata ya Isyesye Jijini Mbeya.
Mazishi yamefanyika machi 1,2025 katika makaburi ya Isyesye na kuhudhuriwa na Viongozi wa UWT Taifa akiwemo Makamu Mwenyekiti Zainabu Shomari,Riziki Kingwande Naibu Katibu Mkuu Taifa na Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson.
Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesili msibani muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Zimbabwe kuiwakilisha nchi katika mkutano wa Kimataifa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara.



0 Comments