Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameongoza mamia ya waumini wa Kanisa la Katoliki Kigango cha Mtakatifu Theresia wa Calcutta Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mtume Mkuu Uyole Jijini Mbeya ambayo imehudhuriwa na Mhashamu Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Mbeya Baba Gervas Nyaisonga.
Katika harambee hiyo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameahidi kuchangia shilingi milioni kumi.
Aidha amewataka Waumini kuunganisha nguvu zao Ili kuhakikisha Kanisa linakamilika kwa wakati.
Ujenzi huo utaanza hivi karibuni baada ya kukamilika makusanyo ya awali ya shilingi milioni mia moja.








0 Comments