Wananchi wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wamesema kuwa hawawezi kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria za nchi zenye viashiria vya kuondoa  amani  ikiwemo maandamano yasiyo na kibali yanayoweza kusababisha vita ambazo zinaendelea baadhi ya Nchi duniani  na kuathiri shughuli za kiuchumi ,kukosekana kwa amani na utulivu  huku watu wakipoteza maisha kwa kuuana ,njaa na wengine  kuishi maisha ya kuhamahama kama wanyama.


Wananchi wilaya ya Rungwe kutoka makundi mbalimbali ikiwemo bodaboda ,wakulima na wafanyabiashara wadogo na wakubwa wametoa msimamo huo baada ya Mbunge mteule wa viti maalum Mkoa wa Mbeya Mh.Suma Fyandomo ambaye amefunga kampeni kwa kutembelea makundi mbalimbali huku akiomba kura za wagombea wa chama chake cha Mapinduzi (CCM) na kutoa elimu ya athari za kutoweka kwa amani kwenye nchi.