Ni muendelezo wa lala salama Kata kwa Kata katika kuhamasisha wanawake kupiga kura.

Oktoba 25,2025 Mbunge mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mahundi ameendelea kutoa elimu na kuomba kura Kata za Mbugani na Kisale Wilaya ya Kyela  akiwaonesha mfano wa karatasi ya kupigia kura kumchagua Rais Mbunge na Diwani  ikiwa zimebaki chache kuelekea upigaji kura uchaguzi mkuu oktoba 29,2025 siku ambayo Serikali imetangaza kuwa ni ya mapumziko ili washiriki uchaguzi bila vikwazo.






"Wanawake wanalo jukumu la kuwaamsha ili kuwaandaa wanaume na wote kwenye familia kwenda kupiga kura" alisema Mahundi.