Sauti kutoka Nyikani
Na Tata Gordon Kalulunga
TAREHE 29/10/2025 yaani siku ya Juma Tano Juma lijalo ndiyo siku ya Watanzania kuwachagua madiwani, Wabunge na Rais wa JMT.
Nikiwa miongozi mwa waandishi wa Habari waandamizi na wachambuzi wa masuala ya siasa na utawala bora nchini, naomba leo uungane nami kuliangazia Jimbo la Mbeya Mjini hasa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Patrick Mwalunenge (Pichani).
Nitakurejesha mwaka 2023 nilipowaambia wana CCM kuwa kwanini Mwalunenge alistahili kupewa kura za ndiyo kuwa Mwenyekiti wao ngazi ya Mkoa.
Tuanzie hapa.
Patrick Mwalunenge anazo sifa kadhaa za kiuongozi zinazoshawishi kumuombea kura bila nishai mbele za watu katika Jimbo la Mbeya mjini.
1. Hana siasa za makundi ndani ya CCM wala kwenye jamii.
2. Ni mtu mnyoofu na mwenye upeo mkubwa wa kutambua na kutatua matatizo ya jamii na mtu mmoja mmoja.
3. Anapenda sana watu bila kujali hali zao na hana historia ya matumizi mabaya ya hasira yaani siyo kiongozi wa kuumiza watu bali ni mtetezi wa watu wote.
4. Hajawahi kuwa katika nafasi za kukalipia au kutishia watu kuwalaza rumande.
5. Hana siasa za itikadi za kikoloni. Yeye watu wote ni sawa kwake.
Hivyo ikiwapendeza wana Mbeya Mjini jitokezeni kwa wingi kupiga kura za ujazo kwa mgombea Patrick Mwalunenge.
0765615858
Katika kuthibitisha nilichokisema hapo juu. Mwezi Novemba mwaka 2024, kiongozi mwandamizi wa Chadema ndugu John Mwambigija pia amewahi kumwelezea ndugu Patrick Mwalunenge nami niliandika katika uchambuzi na waweza kusoma kupitia link ifuatayo... https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=pfbid02DC2MDVMpf19ybkwpA2NBxF7242TGeU4xWnwWMvWToFav78muQJxP7q33K62tnFRml&id=100008971367609&mibextid=Nif5oz

0 Comments