Na Gordon Kalulunga, Mbeya
KESHO ndiyo siku ya kupiga kura za Rais, Wabunge na Madiwani.
Unapozungumzia ongezeko la uzalishaji sukari nchini, unazungumzia mambo yafuatayo;
1. Ongezeko la ajira: viwanda vya sukari peke yake vinachangia moja ya tatu ya ajira zote za kilimo nchini.
2. Unazungumzia ongezeko la pato la Taifa yaani GDP maana Tasnia ya sukari pekeee inachangia zaidi ya asilimia moja ya pato ya Taifa.
3. Unazungumzia ongezeko la pesa za kigeni; kwa maana kuwa tunaokoa matumizi ya pesa za kigeni zilizokuwa zikitumika kuagiza sukari.
4. Ongezeko la pesa kwa wakulima wa miwa; mpaka sasa kwa mwaka wakulima wa miwa wa nje wanalipwa zaidi ya bilioni 105 kwa mwaka direct payment wanapouza miwa yao
5. Ongezeko la kodi
6. Miundombinu ya barabara, mashule na hospitali.
NB: yote haya yamefanywa na serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassani, je mpaka hapa watu wenye akili zao wanaanzaje kumnyima kura? Na hapo nimetaja machache kati ya mengi yaliyofanywa ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia ambaye ni mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

0 Comments