HEKO MBUNGE MWALUNENGE KWA MAWAZO YANAYOSHABIHIANA NA RAIS SAMIA

* Ulianza na Pikipiki na sasa matunzo ya watoto sokoni nchi nzima

Na Tata Gordon Kalulunga Mwaipungu

JUNI 24,2025 niliandika Makala ya uchambuzi kuhusu Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Patrick Mwalunenge kuwq alipokuwa akigombea Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya aliasisi wazo la Pikipiki kwa kila Kata ya chama hicho Mkoani Mbeya na akiwa kwenye utekelezaji chama chake kikatangaza kutoa pikipiki nchi nzima.

Makala ile wachache ikawanunisha kwasababu wanazozijua wenyewe.

Katika kampeni zake za kusaka kura za Ubunge Mhe. Mwalunenge akiwa eneo la stendi ya Kabwe Jijini Mbeya pamoja na mambo mengine alitoa wazo/ahadi ya kujenga majengo ya matunzo ya watoto wadogo wa wanawake wanaofanya kazi katika masoko ya Jimbo hilo.

Baadhi walibeza wazo hilo lakini jana katika hotuba ya kufungua Bunge la 13 Jijini Dodoma, Rais wa JMT Dr. Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine alishangiliwa baada ya kutamka kuwa serikali itafanya jambo hilo kwenye masoko nchi nzima.

 "ili kuwasaidia wanawake wanaofanya kazi kwenye masoko tutaongeza na kuratibu kwa karibu mifuko ya uwezeshaji kiuchumi ili kurasimisha biashara zao ili kuwezesha kukopesheka" alisema Mhe. Rais Samia.

Tutawekeza na kuboresha miundombinu ya masoko, mifumo ya maji safi na maji taka, huduma za Afya na vituo vya matunzo ya watoto kwenye masoko" alisema Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan.

Sauti kutoka Nyikani inampongeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa kuwa na maono yanayosadifu kitaifa.

Alianza na suala la Pikipiki mkoa mzima kwa chama chake likawa la kitaifa, akaja na wazo la matunzo ya watoto kwenye masoko nalo sasa litafanyika kitaifa, ndiyo maana ninasema heko kwa Mheshiniwa Mwalunenge Mbunge mwenye maono ya Maendeleo ya watu na Maendeleo ya vitu.

Karibuni Nyikani 0765615858

Post a Comment

0 Comments