Katikati ya mvutano unaoendelea katika mitandao ya kijami anga ya kikanda, Watanzania wengi, wametoa wito kwa mataifa jirani "kupunguza kelele" na kuheshimu utulivu wa nchi. Kauli hizi zikisisitiza msimamo wa muda mrefu wa Tanzania wa kutopenda vurugu na migogoro.
Maoni ya Watanzania yanaonyesha dhamira isiyoyumba ya kulinda amani, ambayo wanaichukulia kama utajiri mkuu na kipaumbele cha kitaifa.
Amani Kwanza, Drama Baadaye
Maoni kadhaa katika majukwaa ya kijamii yamegusa moja kwa moja tabia ya mataifa jirani, yakieleza kutopendezwa na hali ya mvurugano na ukosefu wa utulivu.
"Hatujazoea vita sisi watuache amani yetu ndio utajiri wetu," alieleza mmoja wa wachangiaji akisisitiza umuhimu wa amani.
Wengine walitaja moja kwa moja kuwa hawataki kuingilia katika hali ya migogoro, wakisema: "Hapa bado hatutaki drama kabisa😂😂 Amani kwanza!”.
Kauli nyingine iliyopata uungwaji mkono mkubwa ilikuwa: "watanzania sio watu wa vurugu, watanzania sio watu wa mkumbo," ikifafanua tabia na maadili ya Kitaifa.
Wito wa Kuheshimu Utulivu
Licha ya kujitokeza kwa hisia za kejeli, wengi walieleza kuwa wanaelewa hali ya ndani ya majirani wao, na hivyo hawatarajii upendo au utulivu kutoka kwao.
Mmoja wa wananchi anayeishi mpakani alitoa maoni ya moja kwa moja: "Mimi naishi mpakani nawajua wao kwa wao tu hawapendani mnategemea watupende sisi😂🙌".
Baadhi ya wananchi walionyesha hisia kali dhidi ya majirani kwa kuwaita “shida,” wakisema: "wale sio majirani wale ni shida kama shida zingine 😢😢🙌".
Jumla ya maoni hayo yanaakisi msimamo wa Watanzania wa kukataa ghasia na vurugu, na kusisitiza kuwa kipaumbele chao cha kwanza ni Tanzania kwanza na utulivu wa ndani.

0 Comments