Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewakilishwa na Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi (Mb), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kushiriki Jukwaa la Tisa la Biashara Barani Afrika, linalofanyika jijini Addis Ababa, kuanzia tarehe 16–17 Februari, 2026.
Kaulimbiu ya Jukwaa:
“Financing the Future of Africa: Jobs and Innovation for Sustainable Transformation”
(“Kugharamia Mustakabali wa Afrika: Ajira na Ubunifu kwa Mabadiliko Endelevu”)
Jukwaa hili la kimkakati linawakutanisha Serikali, Wawekezaji, Wafanyabiashara, Taasisi za Fedha na Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano, na kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika biashara na uwekezaji.
Kupitia ushiriki huu, Tanzania inaendelea kusisitiza dhamira yake ya kuchochea ajira, ubunifu, ukuaji wa viwanda, upatikanaji wa masoko na mitaji, na kuharakisha mabadiliko endelevu ya kiuchumi barani Afrika.




0 Comments