NEEMA YA SAMIA: ASILIMIA 80 YA MIPANGO YA SERIKALI YABEBA VIJANA

Asilimia 80 ya mipango ya Serikali ya Awamu ya Sita  imeelekezwa kuwainua vijana moja kwa moja.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, ameeleza kuwa kipindi  katika kipindi cha siku 100 za mwanzo za uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.hicho kimekuwa muhimu kwa nchi kutoka katika changamoto mbalimbali huku ikiendelea kubaki na amani na utulivu wa hali ya juu. 

Tathmini inaonesha kuwa Rais Samia ametekeleza ahadi nyingi za Ilani ya CCM kikamilifu, ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa wizara inayoshughulikia masuala ya vijana.

Katika kile kinachoonekana kama mkombozi kwa sekta ya ubunifu, Wizara ya Habari imepokea Shilingi bilioni tano mahsusi kwa ajili ya waandishi wa habari, wasanii, na waandaaji maudhui, ikiwa ni sehemu ya Shilingi bilioni 200 zilizotolewa kuwezesha makundi mbalimbali. 

Hatua hii inaenda sambamba na ongezeko kubwa la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, ambayo imepaa kutoka Shilingi bilioni 264 hadi kufikia Shilingi trilioni moja, pamoja na mpango wa Shilingi bilioni 90 kwa ajili ya Zanzibar. 

Katibu Mtendaji wa TNBC, Dk. Godwill Wanga, amewahimiza vijana kujikita zaidi kwenye ubunifu wa kidijiti, akibainisha kuwa mfumo mpya wa Jamii Namba utarahisisha utambulisho na upatikanaji wa huduma za kiuchumi.

Mafanikio haya ya siku 100 yameonekana pia katika sekta ya ajira ambapo jumla ya ajira 53,000 zimezalishwa, zikiwemo ajira 41,500 katika sekta ya umma na 11,500 katika sekta binafsi. 

Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Matiko, amesema kasi hiyo inachochea pato la mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa nchi kuelekea lengo la Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050.

Aidha, maboresho katika sekta ya madini na uwekaji wa mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa nje unazidi kufungua milango ya ajira kwa vijana wengi nchini.

Katika upande wa huduma za jamii, serikali imepiga hatua kubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwafikia zaidi ya kaya 290,000 kupitia bima kwa wasio na uwezo, huku kukiwa na maelekezo madhubuti kuwa hakuna mwili wa marehemu utakaozuiliwa hospitalini kwa sababu ya madeni.

Post a Comment

0 Comments