MAHUNDI AFIKA KIGOMA, AANZA ZIARA KWA KUTOA SALAMU OFISI YA CCM

 

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, leo amewasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi, ambapo ameanza kwa kutembelea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma na kutoa salamu za Serikali kwa viongozi wa chama.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mahundi ameeleza kuwa lengo la ujio wake mkoani Kigoma ni kutekeleza majukumu ya kikazi yanayolenga kuimarisha maendeleo ya jamii, ustawi wa wanawake, watoto na makundi maalum, pamoja na kufuatilia utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali inayosimamiwa na wizara yake.

Aidha, ziara hiyo inatarajiwa kujumuisha kukutana na viongozi wa serikali na wadau mbalimbali, kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma na ustawi wa jamii katika Mkoa wa Kigoma.

Post a Comment

0 Comments