M-NEC MWASELELA: Kheri ya Mwaka 2026 wana Mbeya na watanzania wenzangu

Kwa moyo mkunjufu  ninawatakia kila la kheri  katika kuanza mwaka 2026, ukawe mwaka wa Afya njema kwenu, uponyaji kwa walio wagonjwa, ukawe mwaka wa kuimarika kwa familia, kuimarika kwa uchumi wa familia, ukawe mwaka wa  furaha kwa familia.


"Wapo waliokata tamaa  kwa hatua mbali mbali, Mwaka huu 2026 ukawe mwaka wa kuinuka na kuendelea na safari zao bila kujali miba na mawe yaliyopangwa katika safari, thamani kubwa ikawe ni sisi ni watoto wa Mungu, mfano wa Mungu".

Mungu akatupe subira pale mambo yatakapokuwa tofauti na tunavyotarajia .Mwaka 2026 ukawe ni mwaka wa kuchapa kazi, ukawe ni mwaka wa kutumikia wananchi kwa weledi na matokeo makubwa katika eneo lako.

Ukawe mwaka wa kuhubiri mshikamano, upendo, haki na Amani muda wote,"Neno moja la kukumbuka ni kuwa haitawezekani  watu wote wakakubaliana na kila jambo, hivyo utulivu na subira ni muhimu sana.

 Mwisho si Kwa umuhimu Mwaka 2026 ukawe mwaka wa Neema na Baraka nyingi kwa familia zote "Mungu awape maisha marefu na yenye furaha sana.

 Ndimi Ndele Mwaselela (M-NEC), mwana wa Tanzania kutoka Mkoa wa Mbeya "

Post a Comment

0 Comments