MBUNGE MASACHE KASAKA AKABIDHI HUNDI YENYE ZAIDI YA MILIONI 600 MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU CHUNYA

Mbunge wa Jimbo la Lupa–Chunya, Mhe Masache N. Kasaka, akiwa mgeni rasmi, ameshiriki kugawa hundi ya mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya Tsh 604,500,000/= kwa vikundi 43 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wilayani Chunya.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Kasaka amewahimiza wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha wanarejesha kwa wakati ili kuwapa nafasi wengine kunufaika. Aidha, ameeleza dhamira ya serikali kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, umeme na miundombinu ya barabara.

Katika kuunga mkono jitihada hizo, Mhe. Kasaka amechangia kiasi cha Tsh 2,000,000/= kwa ajili ya shughuli za maji kwa makundi hayo na hafla imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Alhaji Mbaraka Batenga, Katibu Tawala Wilaya Ndugu Anakleth Michombero, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Kelvin Nshishi, Kaimu Mkurugenzi Ndugu Athuman Bamba, Afisa Maendeleo ya Jamii Bi Marieta Mrose, Katibu wa CCM Wilaya Ndugu Jockery Selemani pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wilaya Ndugu Ezelina Mwakisole


KAZI NA UTU — CHUNYA TUNASONGA MBELE! 💪🇹🇿

Post a Comment

0 Comments