Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, ambaye pia ni Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, leo ameshiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru uliowasili Mkoa wa Mbeya ukitokea Wilaya ya Mbarali.
Baada ya mapokezi hayo, Mwenge wa Uhuru umeendelea na safari yake katika Wilaya ya Rungwe, ambapo Mhe. Maryprisca Mahundi ameshiriki katika mbio za Mwenge huo pamoja na viongozi na wananchi wa eneo hilo.
Ushiriki huo ni sehemu ya mwendelezo wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mbeya, zinazolenga kuhamasisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na kuendelea kuimarisha mshikamano na uzalendo nchini.
Mwenge wa Uhuru utaendelea kukimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya shughuli zilizopangwa katika ratiba ya mbio hizo.




0 Comments