HABARI PICHA NA MHE. MAHUNDI

 


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia yaH abari, Mheshimiwa, Mhandisi. MaryPrisca Mahundi (Mb), ametembelea Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Kanda ya Pwani zilizoko Mikocheni, jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Naibu Waziri Mahundi, ametembelea ofisi hizo leo Tarehe 10 Septemba, 2024 kwa lengo la kupata taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kupitia UCSAF.

Mhe. Naibu Waziri amepokelewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi. Peter Mwasalyanda pamoja na watumishi wengine wa Taasisi hiyo.


Post a Comment

0 Comments