*M-NEC MWASELELA ANAONESHA UONGOZI UNAOPENDA HAKI NA THAMANI YA KUHESHIMIANA*

 


Kuelekea Uchaguzi Serikali za mitaa 2024

Na Gordon Kalulunga 

ZIKIWA zimebaki siku Mbili kufungwa zoezi la uandikishaji wapiga kura Wakazi kuelekea Serikali za Mitaa, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Mkoani Mbeya Ndugu Ndele Mwaselela ameonekana akikutana na makundi mbalimbali ya watu na kuhamasisha kwenda kujiandikisha.

Kiongozi huyo pia kupitia vyombo vya habari amesikika akisisitiza neno haki, utu na thamani ya kuheshimiana katika siasa huku akisema kuwa ni muhimu Wanasiasa wote kufuata falsafa ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya 4R.

Mbali na M-NEC Mwaselela kuendelea kuhamasisha watu mbalimbali, viongozi wengine na Wana chama wa CCM pia wanaendelea kupiga mbiu kwa umma kuhamasisha watu kuendelea kwenda kujiandikisha.

Ndugu Mwaselela ameonekana katika Kata za Nsalala na Iwindi Mbeya Vijijini na Kata za Iyunga, Nzovwe na Ilomba Mbeya Mjini huku pia akikutana na wazee wa Wilaya hizo akihamasisha kufanya hima kwenda kujiandikisha kwenye madaftari ya Mkazi bila kujali itikadi za Siasa.

Ziara hizi za M-NEC Ndele Mwaselela zinaonesha ni namna gani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kwenda Sambamba na 4R za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili kurejea katika ushindani wa haki wa siasa za nchi yetu.

Nadhani isingekuwa hivyo, viongozi wa CCM wasingehangaika kuhamasisha kwa nguvu zao zote watu kwenda kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Ndiyo maana ninasema kuwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 M-NEC Ndele Mwaselela anaonesha uongozi  unaojali haki na thamani ya kuheshimiana katika siasa na maisha ya kawaida.

Post a Comment

0 Comments