Na Gordon Kalulunga, Mbeya
MJUMBE wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya Ndugu Ndele Mwaselela amewaasa wagombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wa vyama vyote nchini kutumia ndimi zao vizuri ili kutowagawa watanzania kupitia kampeni zao.
Hayo ameyasema leo Octoba 20, Mwaka huu mbele ya waumini wa Kanisa la KKT Usharika wa ZZK Mbalizi Mkoani Mbeya.
Kiongozi huyo pia amewasihi Watanzania kuendelea kuishi kwa kupendana na kusameheana kama ilivyo falsafa ya 4R za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
M-NEC Mwaselela ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika harambee ya changizo la vyombo vya kuhubiria (Muziki).
"Nitoe Wito pia kuwa sasa tumemaliza kujiandikisha hivyo tuhamasishane kwenda kupiga kura na tukawachague viongozi wenye hofu ya Mungu" amesema M-NEC Mwaselela.

0 Comments