Ni Oktoba 11,2024, Mke wa Mbunge wa jimbo la Lupa (Chunya) Veronica Masache Kasaka (mwenye Skafu) amechangia kiasi cha Fedha Shilingi Milioni Moja (1,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari Itewe iliyopo Chunya Mjini.
Bi. veronica alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha Nne katika shule hiyo.
Mbali na mchango huo Bi. Veronica Kasaka ameendesha harambee ya ujenzi wa uzio wa shule hiyo na kupatikana kiasi cha shilingi Milioni mbili laki tatu na sitini na nne elfu pamoja na mifuko 79 ya saruji yenye thamani ya Mil 1.6. Jumla harambee ya Ujenzi wa uzio imekusanya Tsh Milioni Nne.
CHUNYA INAJENGWA NA WANA CHUNYA.



0 Comments