Na Gordon Kalulunga Mwaipungu
KUTANA na Timida Fyandomo (Aliyevaa kofia ya Kijani). Ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Mbeya.
Ni kiongozi wa Vijana anayemiliki sana Masikio kuliko mdomo, yawezekana pia ndiyo Moja ya nguzo yake ya mafanikio katika Kuta za Siasa za ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni Binti anayependa kujifunza pia ya kale kwa waliomtangulia kwenye siasa.
Jana Octoba 10,2024 amefika katika Eneo la SIDO Mwanjelwa Jijini Mbeya na kukutana na vijana wanaoishi katika Mazingira tata (Mtaani) katika maskani zisizo rasmi.
Vijana hao wakampokea na kuzungumza naye huku akiwahamasisha wale wote ambao Wana miaka 18 na zaidi wajitokeze kwenda kuandikishwa katika Daftari la wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27, Mwaka huu.
Timida pia aliwaasa vijana hao kujiepusha na vitendo na makundi ya kihalifu na uhalifu pia kuepukana na matumizi ya dawa za Kulevya.
Baadae alikula nao chakula na kuahidi kurejea tena kukutana nao ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza huku akisema *Natamani kuona tabasamu katika nyuso zenu, maana yaliyopita si ndwele, tugange yajayo"*
Ndiyo maana ninasema kuwa, Timida Fyandomo anastahili vigelegele kwa kukutana na vijana hao ambao kwa asilimia kubwa jamii imewatenga.

0 Comments