Lupa 📍
Mbunge wa Lupa-chunya Mhe. Masache Kasaka ameambatana na Mhe. Juma Homera mkuu wa mkoa wa mbeya katika ziara ya wilaya ya Chunya lengo kubwa ni kusikikiliza kero za wananchi wa katika kata na vitongoji mbali mbali na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika ziara hiyo Mhe. Masache Kasaka amezungumza na wananchi hao na kupokea kero zao ikiwemo barabara itokayo mwanzo mgumu kuunganisha ngwala itafikishwa kwa Mhe. Samia Suluhu ili iweze kupatiwa ufumbuzi.
Sambamba na hilo Mh Masache kasaka ameshukuru serikali inayoongozwa na Rais Mh Dkt Samia Suluhu kwa namna alivyoweza kutekeleza miradi mbali mbali katika kata hiyo ya nkung’ungu na kuweka mabadiriko ambayo awali hayakuwepo.
KAZI NA UTU
*CHUNYA TUNASONGA MBELE*




0 Comments