Mbunge mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameshiriki mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru Jijini Mbeya.

Mwenge utazindua miradi ya maendeleo Jijini Mbeya kabla ya kuhitimisha rasmi mbio zake katika Uwanja wa Sokoine mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.