DKT. TULIA AWATEMBELEA WANANCHI WALIOPATWA NA JANGA LA MAFURIKO JIMBONI UYOLE

05 Januari 2026. Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole Mh. Dkt.Tulia Ackson amewatembelea wananchi wa kata ya Ilemi na Isyesye waliokumbwa na Mafuriko kipindi hiki cha Mvua nyingi zinazoendelea kunyesha nchini.

Dkt.Tulia ametembelea na kukagua maeneo yote katika kata za Ilemi na Isyesye ambayo athali kubwa imetokea na kuahidi kuwasilisha changamoto hizo kwa serikali ili wananchi  hao waweze kupatiwa msaada wa haraka kabla ya athali hizo kuwa na matokeo makubwa.

Dkt. Tulia amewataka wananchi kutokujenga maeneo ambayo yanachangamoto ya kujaa kwa maji lakini pia kwa wale wanaotupa taka katika mifereji ya maji waweze kuacha tabia hiyo kwani inapelekea mifereji hiyo kuziba na kupelekea maji kuongezeka na kuleta maafa kwa baadhi ya wananchi.

Dkt. Tulia amehitimisha kwa kuwapa pole wananchi wote wa kata hizo hasa waliokumbwa changamoto hiyo kwa kipindi ambacho unatafutwa ufumbuzi wa kutatua changamoto hiyo.

Post a Comment

0 Comments