Kuna usemi usemao "nguvu ya simba ipo kwenye ukimya wake," na kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ukimya wake ni tufani ya maendeleo inayofuta machozi ya wananchi.
Kwa wale wanaodhani uongozi ni kupiga kelele majukwaani, takwimu za Wizara ya Ujenzi na TANROADS ndani ya siku 100 pekee, ni jibu tosha kuwa Mama anatosha na yupo mkali kwenye usimamizi wa kodi za Watanzania. Yeyote anayebisha kuhusu kasi hii, labda akapimwe akili.
Bilioni 500: Ahadi Inayozungumza kwa Vitendo
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameweka wazi kile kinachoitwa "Historia ya King'ori." Ndani ya siku 100, Serikali imemwaga zaidi ya shilingi bilioni 500 kupitia mpango wa dharura wa CERC. Hii siyo namba ndogo; ni fedha iliyokwenda kukamilisha madaraja 40 ya dharura kati ya 81 yaliyopangwa nchini. Hapa ndipo tunapoona ukali wa Rais Samia—haishii kutoa maelekezo, anatoa fedha na kuhakikisha makandarasi wanalipwa ili kazi isisimame.
Mapinduzi ya King'ori: Zaidi ya Barabara ni Utu
Kule King'ori, Arusha, Rais Samia ameweka "Tabasamu la Utu." Ndani ya muda mfupi, amefanya yafuatayo:Amekamilisha madaraja sita makubwa yanayookoa maisha dhidi ya maji ya milimani;ameweka taa 136 za barabarani, akigeuza usiku kuwa mchana kwa usalama wa wananchi.
Pia amejenga kilometa moja ya lami na vituo viwili vya daladala ili kurahisisha maisha ya watu wa hali ya chini.
Huu ndio usimamizi unaogusa maisha ya mtu mmoja mmoja; huku siyo tu kujenga miundombinu, ni kurudisha heshima ya mwananchi.
Ukali wa Rais Samia katika kuleta ufanisi umefika hadi Dar es Salaam. Katika eneo la Rangi Tatu (Mbagala) kuelekea Kongowe na Mkuranga, kero ya foleni iliyodumu kwa miaka sasa inapata dawa. Ndani ya siku 100 hizi ametoa shilingi bilioni 16 kama fidia kwa wananchi ili kupisha ujenzi na amemwaga shilingi bilioni 9 za awali ili kazi ianze mara moja.
Huu ni ushahidi kuwa Rais Samia hataki michezo kwenye miradi ya kimkakati. Anatoa fidia kwa wakati na anatoa fedha za ujenzi kwa wakati.
Ukitazama mafanikio haya unaona kabisa kwamba kuna usimamizi wa chuma kwenye glovu ya hariri kwani Serikali ya Rais Samia ndani ya siku 100 imelipa makandarasi, imejenga madaraja ya dharura, na imefungua njia kuu za uchumi. Kwa fedha hizi (ikiwemo bilioni 280 kutoka Hazina na nyingine kwa wafadhili), ni wazi kuwa Rais ana aminiwa na ana uwezo wa kusimamia rasilimali.
Wanaosema vinginevyo waangalie madaraja ya King'ori na fidia za Mbagala—huko ndiko kura ya maoni ya wananchi iliko. Mama anatosha, na kasi yake haina breki!

0 Comments