Na Gordon Kalulunga, Mbeya
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Patrick Mwalunenge amefika katika Stendi (Kijiwe) cha wamiliki na Madereva wa Gari ndogo maarufu kama Kirikuu Mwanjelwa Jijini Mbeya na kuwasikiliza Mahitaji yao.
Pamoja na mambo mengine, Mheshimiwa Mwalunenge amewaahidi ndani ya Mwezi huu kuwaunganisha wamiliki na Madereva hao na kampuni ya kukopesha gari ndogo ili waweze kukopa na yeye atakuwa Mmoja wa wadhamini wao.
Kiongozi huyo ambaye amejipambanua kuwa mpenda kazi na kuwainua wengine amewasihi wamiliki na Madereva hao ambao wengi wao ni vijana kusajili kikundi Ili iwe rahisi kwao kutambulikabrasmi na kudhaminika.
Mbeya Mjini ni njema, chini ya Mbunge Mheshimiwa Patrick Mwalunenge, atakaye na aje.

0 Comments