Na Jackline Minja, WMJJWM
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Maryprisca Mahundi amewahimiza wanawake Mkoani Mbeya kuendelea kusimama imara kupinga vitendo vya ukatili na kuimarisha malezi bora ya watoto.
Mhe, Mahundi amesema hayo Machi 08, 2026 katika sherehe iliyoandaliwa na kundi la Wanawake wa Dhahabu kutoka Wilaya ya Chunya ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wanawake.
Mhe. Mahundi amesema siku hiyo iwe ukumbusho kwa wanawake juu ya wajibu wao wa kulea na kuwajenga watoto katika misingi sahihi ya maadili, mila na tamaduni za Kitanzania ili waweze kukua wakiwa raia wema na wenye mchango chanya katika jamii.
Katika sherehe hiyo ambapo ilihudhuriwa na Mbunge wa viitu Maalum Mhe. Nassir Ally ameeleza wazazi kutowaficha watoto wenye ulemavu, Kwa kuwa watoto hao wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa kama watoto wengine iwapo watapatiwa malezi bora na fursa sawa katika jamii.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Wilaya ya Chunya, Faima Mohamed amewashukuru viongozi hao kwa kufika na kushiriki maadhimisho hayo.
Aidha, amewahimiza wanawake kuendelea kupaza sauti kupinga vitendo vya ukatili katika jamii, akieleza kuwa wakati mwingine wanawake wenyewe wamekuwa wakisahau wajibu wao wa kulinda na kusimamia maadili ndani ya familia na jamii.





0 Comments