WANANCHI WAPINGA SHINIKIZO LA MAANDAMANO: WAONYA ULAGHAI WA WANAHARAKATI WA NJE, WAHIMIZA NJIA YA MARIDHIANO


Wimbi la mabadiliko ya kifikra limezidi kushika kasi miongoni mwa Watanzania, ambapo kwa sasa kundi kubwa la wananchi na wajasiriamali limejitokeza hadharani kupinga kile kinachoitwa "maandamano ya kurubuniwa." Wananchi hao wamewataka watu wanaochochea vurugu wakiwa nje ya nchi, akiwemo mwanaharakati Maria Sarungi (anayefahamika pia kama 'Manywele' kwenye mijadala ya mitandaoni), kuacha mara moja kuwahadaa Watanzania kwa maslahi binafsi.

"Tuache Kutumika kama Ngazi" Kupitia maoni mbalimbali ya wananchi (kama yanavyoonekana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari), ujumbe umekuwa mmoja: "Kudai haki bila kufuata sheria ni kufanya fujo." Wananchi wamehoji kwa nini wanaochochea maandamano hawakai mstari wa mbele na familia zao, badala yake wanatumia vijana wa kipato cha chini kama kinga ya vurugu.

"Siasa yetu ni amani na biashara. Wale wanaotuambia 'nendeni' badala ya 'twendeni' hawana nia njema na mustakabali wa taifa letu," alieleza mmoja wa wachia maoni akirejea kauli za viongozi wa maandamano hayo.

Watanzania wameaswa kuachana na lugha za kejeli, matusi, na chuki dhidi ya viongozi. Badala yake, wametakiwa kufuata Taratibu za Maridhiano zinazoshughulikiwa na Tume zilizopo ili kupata ufumbuzi wa kero mbalimbali nchini.

Kwa kuwa hakuna nchi iliyopata maendeleo kupitia barabara zilizovunjika na miundombinu iliyoharibiwa,wananchi wenye kero wanaombwa kuziwasilisha kupitia njia rasmi za kisheria ili serikali na tume husika zipate taarifa sahihi na kuzifanyia kazi bila kuvunja amani.

Aidha wananchi hao wameiomba mamlaka za ulinzi na usalama kusimamia sheria kwa ukamilifu ili kulinda amani ya nchi. Ujumbe kwa 'Manywele' na wenzake ni mmoja: "Imetosha! Watanzania wameamka na sasa wanachagua meza ya mazungumzo na maridhiano badala ya barabara za fujo na chuki."

Post a Comment

0 Comments