AONAVYO M-NEC MWASELELA DIPLOMASIA NA UMOJA WA KITAIFA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA


Na Gordon Kalulunga

WAKATI Rais Samia Suluhu Hassan akitimiza miaka Mitatu tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 19,2024, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu Ndele Mwaselela kutoka Mkoa wa Mbeya amechambua mafanikio ya uongozi wa Rais Samia katika Sekta mbalimbali.

Kiongozi huyo amesema kuna mafanikio makubwa katika masuala ya Diplomasia na Umoja wa Kitaifa.

Anakumbusha kauli ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakati anaapa alitamka kuwa ataanza na suala la Kuifungua nchi.

"Ustahimilivu, kujenga watu kuwa wamoja, hili halina ubishi na kama kuna zawadi ya kuwa kuna Rais anastahili kupata Tuzo duniani ya kuboresha demokrasia basi anayestahili ni Rais Samia Suluhu Hassan " amesema Ndele Mwaselela.

Kwamba Rais Samia aliahidi Kuifungua nchi na ameonesha kwa vitendo kwa kuboresha siasa za Diplomasia za nje ya nchi na ikikumbukwa kuwa wakati fulani tulikuwa na shida na baadhi ya majirani lakini Rais Samia alipoingia madarakani akawafuata na sasa utengamano umerejea.

"Kwa muda mfupi aliokaa madarakani kweli nchi kaifungua kwa kujenga mahusiano mazuri na nchi zingine na anapofanya hivyo anaiaminisha nchi kuwa ipo salama katika uwekezaji nk"  anasema.

Anaeleza kwamba, ili wawekezaji waje kuwekeza nchini lazima wajiridhishe kama kuna siasa safi na kwamba kwa sasa kila mmoja anaona.

USHAURI.

Ameshauri kuwa ikimpendeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kufanya mabadiliko ya Watendaji kwasababu wapo baadhi ambao bado hawajajua mbio za Mheshimiwa Rais.


"Na Mimi kwasababu ni kiongozi, niendelee kuwaelekeza viongozi ngazi za mikoa, Wilaya na Kata waelewe kuwa tunaposema 4R ni 4R, hivyo lazima tuvumiliane" amesema M-NEC Mwaselela kutoka Mkoa wa Mbeya.

Post a Comment

0 Comments