Mapema Julai 16, 2024 Mbunge wa Jimbo la Lupa-ChunyaMkoani Mbeya Mhe. Masache Kasaka ameendelea na ziara yake katika Kata ya Mafyeko kwa kutembelea vitongoji vya Idodomia na Tulieni. 

Katika ziara hiyo Mhe Masache aliambatana na Kaimu Katibu CCM wilaya ya chunya ndugu Zaituni Sembo, Mjumbe K/siasa Mzee Mwileky na Diwani wa Mafyeko Mhe. Kamaka na kukagua ujenzi wa shule Shikizi Idodomia iliyopokea zaidi ya Mil 59.6 na Shule ya Msingi Tulieni iliyopokea zaidi ya Milioni 123 na kupata usajili mwezi Juni 2024.

Sambamba na hilo Mh.Masache N,Kasaka amefanya  mikutano na Wananchi katika Vitongoji Viwili Idodoma na Tulieni kwa lengo kuwapa mrejesho wa bungeni na  kupokea kero za wananchi na baadhi ziliweza kupata ufumbuzi toka ka Mh mbunge.

Mhe Mbunge ameendelea kumshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kutoa Fedha za Maendeleo wilayani Chunya

SAMIA NA MASACHE

CHUNYA KAZI INAENDELEA