HIZI NDIZO ALAMA 7 ALIZOZIACHA M-NEC MWASELELA ZANZIBAR JULAI 2024

 Sauti kutoka Nyikani

Na Gordon Kalulunga 

HISTORIA uandikwa na kusimuliwa.

Ipo Historia Moja ambayo nimeona nikusimulie kutoka Zanzibar ambayo inamhusu Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mbeya Ndugu Ndele Mwaselela.

Ipo hivi

Leo Julai 16,2024 Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu Ndele Mwaselela amehitimisha ziara yake ya siku Nne Visiwani Zanzibar na kuacha tabasamu kwa wakaazi.

1. Alikagua shughuli mbalimbali za Maendeleo yaliyofanywa na Serikali inayoongwa na Rais Dkt. Hussen Mwinyi ikiwemo kujionea huduma za Hospitali ambapo wagonjwa walieleza wazi kuwa wanatibiwa bure na kupatiwa chakula mara Tatu kwa siku yaani *bure ya ukweli* na kila Kitanda kina sehemu ya mawasiliano ya mgonjwa na Daktari.

Kiongozi huyo pamoja na kupongeza jitihada hizo zilizousuza pia moyo wake hakuacha kulitaja jina la Rais Mwinyi na kuwasihi wananchi kuendelea kumuunga mkono na kuunga mkono chama chake huku akikumbuka msemo wa wahenga usemao Moyo usio na shukrani haufai kuwa sehemu ya mwili wa binadamu.

2. Alitoa hamasa kwa Vijana kwa kuanzisha ligi ya Mpira wa miguu na kutoa mipira 10 na Jezi Jozi 10 huku akiahidi kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 4 kama zawadi kwa washindi.

Ligi hiyo inaenda kwa jina la *Dkt. Mwinyi Mshikamano CUP*.

3. Alikutana na Mabalozi wa CCM na kuzungumza nao.

4. Amejitolea kukarabati Ofisi ya wadi (Kata) ya Dimani.

5. Ametoa vifaa vya (TEHAMA) Computer na simu kwa ajili ya usajili wa Wanachama wa CCM kidigiti.

6. Ametoa tofali zote zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa afisi (Ofisi) ya Wilaya ya Diwani.

7. Ametoa ufadhili kwa mwanafunzi mmoja wa kike katika masomo ya Chuo kikuu.

Moja ya zawadi/kipaji alichotunukiwa M-NEC Ndele Mwaselela ni kwamba anao mkono wa utoaji na kila anapokanyaga huwa anaacha tabasamu katika kuiletea jamii Maendeleo ya watu na Maendeleo ya vitu.

Hii ndiyo Simulizi ya leo kuhusu alama 7 alizoziacha M-NEC Ndele Mwaselela katika ziara yake ya siku 4 Zanzibar.

Naomba kutoka hoja.


0765615858

Post a Comment

0 Comments