TUJISIFU KUUPIGA MWINGI KWA KUBADILI MAISHA HALISI YA WATU

 Sauti kutoka Nyikani


Na Gordon Kalulunga 

UTANGULIZI

*MTU asiye na pesa Taslimu ni masikini kama Ndege wa mwituni.*

.................

Nimeona nianze na utangulizi huo ndipo tuungane mioyo ya kutafakari yafuatayo.

AFYA.

Mtaji wa mtu hapa duniani ni Afya, mtu asiye na uhakika wa kumudu kununua matibabu hatuwezi kumuweka katika kundi la watu walioendelea au wanaoendelea.

Tujiulize kuwa je ni Watanzania wangapi wanaomuda gharama za biashara za matibabu?

Pia tujiulize kuwa je rasilimali zetu hapa nchini haziwezi kutiba watu wetu?

Maswali ni mengi sana.

Unaweza kujiuliza kuwa kwanini nimegusa jambo hili?

Jawabu lake ni dogo tu ni kwamba rasilimali za Taifa haziwezi kufanya kazi bila rasilimali watu.

Ukiangalia rasilimali zilizopo ndani ya nchi yetu hazihusiani Moja kwa Moja na kasi ya tukiitacho Maendeleo tuliyonayo.

Mfano unapokuwa na Madini, ni muhimu kuyagauza Madini hayo kuwa Barabara, Hospitali, Maji, Umeme lakini yote hayo hayawezi kuwa Maendeleo kama watu wetu hawana Afya njema na hawawezi kumudu gharama za matibabu.

Tunawahitaji binadamu wa kugeuza rasilimali za Taifa letu kuwa maisha kamili ya watu kwa kila siku siyo nyakati za uchaguzi tu.

Mfano Kuna Miradi inayotekelezwa hasa kwa masuala ya miundombinu, je wananchi wanapata vipato kupitia hiyo Miradi? 

Msomaji wangu wa Kamala hii, naamini upo mradi unaotekelezwa karibu na eneo ulilopo, je unapata kipato chochote kupitia mradi huo? Jibu unalo.

Nadhani ipo haja ya kutafsiri Maendeleo yetu bila kuiga.

USHAURI WANGU

*Sisi Tanzania tunaweza kusema kuwa tafsiri ya Maendeleo yetu ni kila Mtanzania kugharamiwa matibabu kwa kuwa na Bima ya Afya tofauti na sasa tunaona kwenye Afya ni kuwa na maandishi yasemayo watoto chini ya miaka Mitano watatibiwa bure*.

Ndani ya Matibabu bure kwa wote tunaweza kuongeza kuwa kila Mtanzania awe na Maji safi na salama, umeme, Shule bure kuanzia Msingi mpaka Chuo kikuu.

Mambo haya yawekwe kwenye Katiba ili Katiba yetu isihatarishe Maendeleo yetu kama sasa ambapo kila Rais anayeingia madarakani anafanya jambo lake kwa mgongo wa Ilani hata asipotekeleza yaliyomo kwenye Ilani hakuna wa kumuuliza maana yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Zaidi tupate watu wema ndiyo wawe viongozi maana kwa nchi zetu za Afrika zinaongozwa na dhamira za wanaokuwepo muda huo maradakani na ndiyo maana ninasema kuwa tusifiane kuupiga mwingi kwa kubadili maisha halisi ya watu kupitia rasilimali zetu vinginevyo tuone aibu mbele ya (Nuru) ya umasikini unavyoongezeka kwa watu wetu huku tukijisifu kuhusu miundombinu na kusema tunaupiga mwingi. 

0765615858

Post a Comment

0 Comments