M-NEC MWASELELA ANATAFSIRI MAONO YA RAIS SAMIA KWA VITENDO


 Sauti kutoka Nyikani 

Na Gordon Kalulunga 

MOJA ya jukumu na kazi za Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC) ni pamoja na kutoa uongozi wa Siasa ya CCM kwa jumla kwa Tanzania nzima, uwezo wa kubuni, kujadili, kuamua na kutoa Miongozo ya Siasa ya CCM katika mambo mbalimbali.

(2) Kueneza Itikadi na Siasa ya CCM, kuongoza mafunzo ya Siasa ya CCM na kukuza nadharia na Itikadi ya CCM ya Ujamaa na Kujitegemea.

Tuanzie hapa

Ndele Mwaselela ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mbeya.

Ni kiongozi kijana mwenye uwezo mkubwa wa kutafsiri kwa vitendo maono ya Mwenyekiti wake wa CCM Taifa na kuwafikishia wananchi nchi nzima.

Hivi karibuni kafanya ziara zake katika Wilaya ya Mbeya Vijijini pamoja na Visiwani Zanzibar.

Mbeya Vijijini pamoja na mambo mengine kafanikisha kuwaweka pamoja vijana wa Wilaya nzima kwa kuwaanzishia Ligi ya Mpira wa miguu inayojulikana kwa jina la Dr. Samia Mbeya DC Mshikamano CUP.

Ligi hiyo itagharimu zaidi ya Shilingi Milioni 18 na tayari timu zote 16 zimepewa Jezi na Mpira..

Njia hii naiona ni Moja ya njia Bora ya kuwafikia watu na kueleza mambo yanayotekelezwa na Rais Samia na kuhamasisha watu kujua umuhimu wa kuchagua viongozi wenye ushupavu wa uongozi.

Ligi hiyo ambayo ipo katika hatua ya Timu 16 Bora inaendelea katika uwanja wa Jeshi Mbalizi.

Katika hatua nyingine, M-NEC Ndele Mwaselela amefanya ziara Wilaya ya Mjini Visiwani Zanzibar na kuanzisha ligi ijulikanayo kwa jina la Dkt. Mwinyi Mshikamano Malindi Cup, lengo ni kukuza michezo lakini pia kuwezesha Watanzania kukutana hali ambayo inaongeza mzunguko wa fedha mtaani na Mshikamano wa jamii.

Ndiyo maana ninasema kuwa, M-NEC Mwaselela anatafsiri maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa vitendo.

Naomba kutoa hoja.

0765615858

Post a Comment

0 Comments