NI Julai 27, 2024 Mbunge wa Jimbo la Lupa-Chunya Mkoani Mbeya, Mheshimiwa Masache N. Kasaka, amefanya ziara katika Kata ya Kasanga Vitongoji vya Mabatini na Kivukoni ambapo alitembelea Ujenzi wa Madarasa Sita shule Mpya ya Sekondari Kasanga ambapo wananchi walishajenga msingi na Mhe. Masache aliwapatia Tsh. Milioni Nne kuendelea na Ujenzi huo.
Sambamba na hilo Mh.Masache N,Kasaka ametembelea Mradi wa Maji Kijiji cha Soweto uliogharimu Tsh. Milioni 383, Mradi huo umefadhiliwa na shirika la CRS.
Mheshimiwa Masache amemshukuru diwani wa kata ya Kasanga Mheshimiwa Benson Msomba kwa usimamizi mzuri wa miradi.
KATIKA ziara hiyo Mheshimiwa Masache Kasaka akiambatana na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Chunya ndugu Yusuph Libaba, Mhe. Diwani Kata ya Itewe Mhe. Alex Kinyamagoha, Mhe. Benson Msomba na Kaimu K/Katibu CCM Wilaya Ndg. Maendeleo R.Nyamka.
SAMIA NA MASACHE.
CHUNYA KAZI INAENDELEA.





0 Comments