M-NEC MBEYA ANASTAHILI JINA LA MWASELELA AHADI UMEPATA


 Sauti kutoka Nyikani 

Na Gordon Kalulunga 

Ndele Jailos Mwaselela ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC, ameziamsha siasa za Mkoa wa Mbeya ambazo zililala hasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Siasa anazozifanya ni Siasa za uamsho ambazo zinasaidia wananchi wa hali ya chini hata ambao siyo wajumbe.

Hivi karibuni ziliibuka siasa za mpe yeye na CCM ilikuwa kama chama cha Wajumbe pekee, lakini Ndugu Mwaselela anakipeleka chama kwa watu wote.

Katika ziara yake Jimbo la Mbeya Vijijini alisikiliza kero na kuzitatua papo kwa papo na zingine kuahidi kuzitatua kwa vitendo.

Baadhi wakabeza ahadi zake na kwamba hatoweza kuzitekeleza.

Jana Juni 17,2024 amewaumbua kwa vitendo kwa kutekeleza ahadi aliyoiahidi Juni 15,2024 kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni Tano kwa ajili ya Taa za stendi ya Tarafani Mbeya Vijijini na kukabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Leo Juni 18,2024 ametekeleza ahadi zingine mbili kwa kukabidhi Mabati Bando Tano zenye thamani ya Milioni 2 kwa ajili ya shule shikizi katika Kata mbili za Mwabowo na Kata ya Ihango ambako wananchi walimuomba.

Bati hizo amezikabidhi akiwa katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Mbeya zilizopo eneo la Soko Matola.

Sanjali na Utekelezaji wa ahadi hiyo, pia ametekeleza ahadi ya kiasi cha Shilingi Lakini 6 aliyowaahidi watenda kazi wanaoopoa mchanga katika Mto Mbalizi kwa ajili ya ununuzi wa Mashine ya kutozea ushuru.

Ndiyo maana ninasema kuwa, M-NEC wa Mkoa wa Mbeya anastahili jina la Mwaselela ahadi umepata.

Naomba kutoa hoja.


0765615858

Post a Comment

0 Comments