MIKONO YA MWASELELA ILIVYOKABIDHI MILIONI 5 STENDI MBALIZI KWA NIABA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN


-Aitwa Mwaselela ahadi umepata.

Na Gordon Kalulunga

TAREHE 15/06/2024 akiwa katika stendi ya Tarafani Mbalizi Wilaya ya Mbeya, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC Ndugu Ndele Mwaselela aliahidi kuwapatia Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya taa 10 kwa ajili ya stendi hiyo iliyopo Makao Makuu ya Mwonekano wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Ahadi hiyo ilitokana na Wananchi kumpatia kero ya giza katika eneo hilo ikiwemo vyoo vya stendi hiyo kufungwa saa 2 Usiku.

Leo Juni 17,2024 Ndugu Mwaselela kapatiwa jina jipya na kuitwa Mwaselela ahadi umepata baada ya kukabidhi kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000) kwa ajili ya ununuzi wa taa 10 za stendi hiyo ambayo ina changamoto pia ya kutokuwa na sehemu maalum ya abiria kupumzikia.

M-NEC Mwaselela amesema kiasi hicho cha fedha amekitoa kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anapenda wananchi wapate raha katika nchi yao.

"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda wananchi wake wapate raha hivyo kanituma nitoe kiasi hiki cha Shilingi Milioni Tano kwa ajili ya stendi hii ya Tarafani hapa Mbalizi ili kutowesha giza na mfanye biashara zenu saa 24" amesema M-NEC Mwaselela.

Akipokea kiasi hicho cha fedha kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Ndugu Wazidi Mahenge amemshukuru kiongozi huyo na kuahidi kuwa taa hizo zitawaka ndani ya siku 7 kuanzia leo Juni 17,2024.

"Mheshimiwa M-NEC tunakushukuru na kukuahidi kuwa ndani ya siku 7 taa zitaanza kuwaka na hakika ziara yako hapa Mbeya DC imeleta matunda makubwa sana na tunakuomba urudi tena na tutakupa ushirikiano" amesema Mahenge.

Afisa Mtendaji wa Mji mdogo wa Mbalizi, Daudi Mbembela licha ya kuungana na viongozi wenzake kushukuru kwa jambo hilo, pia ameuvunja uongozi wa stendi hiyo kuanzia leo.

Kwa upande wao watenda kazi ndani ya stendi hiyo mbali na shangwe na vifijo, wameahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiletea Maendeleo Tanzania.

Martin Benela na Tuku Mwamanda wamemuomba M-NEC Mwaselela kuwa huko mbeleni akihitaji nafasi nyingine yeyote asisite kuwashirikisha na kwamba uchaguzi ujao kura zao watampatia Rais Samia.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbalizi Ndugu Paul Mwampaka amemshukuru kiongozi huyo na kwamba ndiye kiongozi pekee aliyekubali kuchangia pesa za mafuta ya mitambo kutengeneza Barabara ya kwenda katika eneo la maziko baada ya viongozi wengine kukataa kuchangia jamii ya Wana Mbalizi.

Mama Lishe maarufu kwa jina la Mama Alvin Mboga 7 amemshukuru kwa ajili ya taa hizo na kumuomba M-NEC Mwaselela kukutana nao akipata muda jambo ambalo kiongozi huyo amekubali na kuahidi kukutana nao na kuwaongezea mitaji yao.

Hivi ndivyo mikono ya M-NEC Mwaselela ilivyokabidhi Milioni 5 kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika stendi ya Mbalizi Wilaya ya Mbeya leo June 17,2024.

0765615858

Post a Comment

0 Comments