NDELE MWASELELA NI KAMA NYOTA YA MAMA JUSI MBEYA VIJIJINI IFUATWE



Na Gordon Kalulunga 

NILIWAHI kuandika siku za mgongoni kuwa Moja ya sifa ya kiongozi ni kukimbiliwa siyo kukimbiwa.

Ziara ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu Ndele Mwaselela katika Jimbo la Mbeya Vijijini imeonesha siasa za makimbilio kama ile Simulizi ya nyota ya Mama Jusi.

Mwaselela kila alipokanyaga kwa siku 10 amekuwa kimbilio la watu kwasababu ya utashi wake wa kutatua kero za watu bila kujali itikadi za vyama vya siasa na kero nyingi zilikuwa ni za kijamii.

Ziara yake imeonesha siasa wazitakazo wananchi wa Jimbo hilo huku makundi sogozi Wilayani humo nayo kwa tathimini wajumbe wake walio wengi wanaungana na siasa azifanyazo kiongozi huyo huku mtaani nako kukiwa kumekucha.

Mbali na Kata zingine, M-NEC Mwaselela amewezesha kufungwa taa za stendi ya Mbalizi iliyopo Kata ya Utengule Usongwe jambo ambalo lilikuwa Moja ya hitaji muhimu kwa watumiaji wa stendi hiyo.

Pili amewezesha mafuta ya mitambo ya kutengeneza Barabara kwenda kwenye eneo la Maziko ya watu wa Mbalizi ambapo kiongozi wa eneo hilo Ndugu Paul Mwampamba hivi karibuni alitamka hadharani kuwa ni kiongozi pekee aliyekubali kuchangia jambo hilo baada ya viongozi wengine waliopo ndani ya Jimbo hilo kukataa.

Mambo haya machache ndani ya mengi yanaonesha ni namna gani kiongozi huyu ambavyo amekuwa kama nyota ya Mama Jusi Mbeya Vijijini huku kila mawio na machweo akipata zawadi za shukrani kutoka katika makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa mila yaani Machifu kutokana na kurunzi lake la uongozi.

Naomba kutoa hoja.

0765615858

Post a Comment

0 Comments