M-NEC NDELE MWASELELA AMEPELEKA FURAHA MBEYA VIJIJINI


 Sauti kutoka Nyikani 

Na Gordon Kalulunga 

ILI jamii iitwe imeendelea ni muhimu watu wakawa na mambo Mawili ambayo ni Maendeleo ya vitu na Maendeleo ya watu.

Ja Julai 11,2024, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu Ndele Mwaselela, amekabidhi Jozi 16 za Jezi za Mpira wa miguu kwa timu 16 zinazoendelea na ligi iitwayo Dr. Samia Mbeya DC, Mshikamano CUP katika Jimbo la Mbeya Vijijini.

Pamoja na Jezi hizo, kila timu pia ilipatiwa Mpira mmoja mmoja.

Washindi wa Ligi hiyo watapata kitika cha Shilingi Milioni Kumi na Nane (18,000,000) zinazoonekana, mbali na gharama za uendeshaji.

Mbali na vifaa hivyo vya michezo, hivi karibuni M-NEC Mwaselela alipofanya ziara ya uchechemuzi wa Maendeleo katika Jimbo hilo, pamoja na mambo mengine aliwezesha Taa za stendi ya Tarafani Mbalizi ambapo kulikuwa na giza Totoro.

Taa hizo alitoa kiasi cha Shilingi Milioni 5 hadharani.

Nadhani kwa mwana Siasa mzuri wa nyakati hizi hii ni namna Bora ya kukutana na wananchi kwa kuwapa furaha badala ya kuishia kukagua Miradi inayotekelezwa na serikali.

Wananchi wa sasa wanahitaji uwezeshwaji siyo brabra ambazo wanajua kuwa hata usipokuwepo wewe katika nafasi fulani Miradi itatekelezwa tu kufuatia mipango ya Serikali ya nchi mzima na iliyopo ndani ya Ilani za uchaguzi.

Ndiyo maana ninasema kuwa M-NEC Ndele Mwaselela amepeleka furaha Mbeya Vijijini.

Naomba kutoa hoja.

0765615858

Post a Comment

0 Comments