Naibu Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameendelea na ziara yake Jijini Dar es Salam kuzitembelea Taasisi ambazo zipo chini ya Wizara na leo Julai 18,2024 amefika ofisi za Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) na kupata maelezo ya jinsi wanavyohudumia wananchi.
Kwa upande wake Mahundi amewapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwahudumia wananchi na kuwasisitiza kuendelea kuchapakazi kwa uweledi mkubwa huku akiwaahidi kushirikiana kuzitatua changamoto zao.
Aidha amesema Wizara itaendelea kuzifanyia kazi kwa ukaribu changamoto zote zitakazowasilishwa Wizarani.











0 Comments