Sauti kutoka Nyikani
Na Gordon Kalulunga
MEI 28,2024 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu Ndele Mwaselela alitangaza kuwa atahusika kuwasaidia wanafunzi ambao Wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia chakula hasa wale waliopo katika Madarasa ya mitihani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Kauli hiyo imeleta mtanziko na mgagaziko kwa baadhi ya wanasiasa walio chini ya miaka 18.
Jambo hilo likitekelezwa na kiongozi huyo litakuwa jambo jipya kwa siasa za Mkoa wa Mbeya nadhani kwa upya huo ndipo tatizo linapoanzia kama Utekelezaji mpya wa majukumu ayafanyayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda.
Inawezekana asiweze kufikia kila shule lakini kwa kipindi ambacho nimemfahamu naamini Ndugu Mwaselela ataweza kutekeleza hiyo ahadi yake.
Naamini Ndugu Mwaselela amefanya utafiti na kugundua kuwa kutokana na maisha ya wananchi wetu, kuna wanafunzi ambao hawana hata viatu kwa baadhi ya shule.
Mfano mzazi mwenye watoto Tisa ambao wote wanasoma kwa baadhi ya Wazazi ni ngumu sana kumudu gharama za michango ya vyakula shuleni, hivyo jambo hili liwe kama kurunzi kwa serikali kuona namna hali ya maisha ya watu wake licha ya kuwepo mifumo ya Kaya masikini maarufu kama TASAF.
Zipo Kaya zenye umasikini uliotopea ingawa kusema inakuwa kama Uhaini katika nchi.
Niwakumbushe wasomaji wangu kuwa Desemba 2023, Paradise Mission Pre and Primary School ya Mbalizi Mbeya inayoongozwa na Ndugu Mwaselela waliwafikia wazee wasiojiweza katika Kata zote za Jimbo la Mbeya Vijijini ambako ndiko sasa ametangaza kusaidia wanafunzi walioko shuleni hasa shule za umma.
Nilichojifunza ni kwamba watu wenye nguvu ukiwapa Posho wanaona ni haki ila ukitoa kwa masikini kelele zinaibuka.
Ndiyo maana ninasema kuwa Ndele Mwaselela anafanya yasiyozoeleka Mbeya Vijijini ndiyo maana kelele na Mashaka vinaibuka.
0765615858
31/05/2024

0 Comments